MwanzoEUR / BTC • Sarafu
add
EUR / BTC
Bei iliyotangulia
0.000019
Habari za soko
Kuhusu Yuro
Euro ni sarafu ya pamoja katika baadhi ya nchi za Ulaya. Wakazi wake 350,000,000 wanatumia kwa kawaida pesa hiyo. Watu wengine 210,000,000 wanatumia pesa zilizoungwa na euro, hasa barani Afrika.
Tangu mwaka 2002 nchi 13 za EU zilifuta sarafu ya kitaifa ili kutumia Euro tu. Siku hizi ni 20.
Euro moja imegawanyika katika senti 100.
Kuna benknoti za € 5, € 10, € 20, € 50, € 100, € 200, € 500.
Kuna sarafu za metali 8 za € 0,01, € 0,02, € 0,05, € 0,10, € 0,20, € 0,50, € 1, € 2.
Pesa ya karatasi inatolewa na benki kuu ya Ulaya na ni sawa kote.
Sarafu zinatolewa na nchi wanachama na zinatofautiana upande mmoja, lakini sarafu zote hutumika kote. WikipediaKuhusu Bitcoin
Sarafu ya Bit ni mfumo wa malipo dijitali ambao unatumiwa na mamilioni ya watu bila msimamizi wa juu kama Benki Kuu ilivyo katika nchi mbalimbali. Sarafu hiyo huweza kutumika kwa kubadilishana na sarafu nyingine, bidhaa au huduma.
Sarafu ya Bit ilianzishwa na mtu asiyejulikana au kikundi cha watu chini ya jina la Satoshi Nakamoto na kutolewa kama programu huria mwaka 2009. Kuanzia Februari 2015, wafanyabiashara zaidi ya 100,000 wanakubali Sarafu ya Bit kama malipo.
Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Cambridge wa mwaka 2017, kuna watu kati ya milioni 2.9 hadi 5.8 wanaotumia malipo dijitali na wengi wao wanatumia sarafu ya bit.
Mara nyingi sarafu ya bit inaitwa "pesa ya dijitali" lakini wataalamu wengi huiona si pesa bali bidhaa ya bahatisho. Paul Krugmann pamoja na wapokeaji wengine wa Tuzo ya Nobel ya Elimu ya Uchumi aliita udanganyifu akiilinganisha na bahatisho la vitunguu vya maua ya tulip huko Uholanzi katika karne ya 17. Wikipedia