MwanzoJPY / KES • Sarafu
add
JPY / KES
Bei iliyotangulia
0.86
Habari za soko
Kuhusu Yen ya Japani
Yen ni pesa nchini Japani. Alama yake ya kimataifa ni ¥ lakini Japani penyewe huandikwa 円. Yen imekuwa pesa inayotumiwa sana duniani baada ya dolar na euro.
Pesa hii ilianzishwa mwaka 1871 na serikali ya Meiji ikifuata mifano ya pesa za Ulaya. Mwanzoni ililinganishwa na gramu 1.5 za dhahabu.
Thamani ya pesa ilishuka wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na baada ya vita kiwango chake kwa dollar ya Marekani kiliweka kwa ¥360 kwa US$1. Mwaka 2008 ilikuwa ¥104 kwa US$1.
Tangu kuimarika kwa uchumi wa Japani Yen imekuwa pesa muhimu duniani.
Kuna noti za Yen 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000. WikipediaKuhusu Shilingi ya Kenya
Shilingi ya Kenya ni fedha za Kenya. Shilingi moja imegawanywa kwenye senti mia moja.
Shilingi ya Kenya ilianzishwa mwaka 1966 baada ya kuvunjwa kwa bodi ya fedha ya Afrika ya Mashariki iliyosimamia fedha ya pamoja ya Kenya, Tanzania na Uganda iliyoitwa East African Shilling iliyotumiwa katika maeneo yote yaliyokuwa chini ya Uingereza katika Afrika ya Mashariki.
Kuna sarafu za shilingi 1, 5, 10, 20 na 40.
Sarafu za senti zipo za zamani za senti 1, 5, 10, 20 na 50 lakini hazinunui kitu tena.
Noti zilitolewa za shilingi 5, 10, 20, 50, 100, 200, 500 na 1000 ingawaje noti za shilingi 5, 10 na 20 ni nadra sana kuonekana.
Shilingi 1 = Senti 100
Majina ya zamani:
Thumuni 1 = Senti 50
Peni 1 = Senti 10
Ndururu 1 = Senti 5 Wikipedia