Kiendelezi cha Chrome cha Zana za Kuingiza Data za Google

Kiendelezi cha Chrome cha Zana za Kuingiza Data za Google huruhusu watumiaji kutumia zana za kuingiza data kwenye ukurasa wowote wa wavuti katika Chrome. Ili kutumia kiendelezi cha Chrome cha Zana za Kuingiza Data za Google, fuata hatua hizi:

  1. Sakinisha Zana za Kuingiza Data za Google
  2. Bofya ikoni ya kiendelezi na uchague "Chaguo za viendelezi"
  3. Katika ukurasa wa "Chaguo za Viendelezi", chagua zana ya ingizo unayoitaka kutoka kushoto kwenda kulia.
  4. Bofya mara mbili upande wa kushoto ili uongeze zana ya kuingiza data. Bofya mara mbili upande wa kulia ili uondoe kilichochaguliwa.
  5. Panga zana za kuingiza data zilizochaguliwa kwa kubofya zana ya kuingiza data upande wa kulia, na kubofya ikoni za kishale cha juu na kishale cha chini.

Ili utumie zana ya kuingiza data, bonyeza ikoni ya kiendelezi. Katika orodha kunjuzi itakayotokea, chagua zana ya kuingiza data unayoitaka. Zana ya kuingiza data ikiwa imewashwa, kitufe cha kiendelezi kitakuwa ikoni ya rangi kamili, kama vile . Zana ya kuingiza data ikizimwa, kitufe huwa kijivu . Kubofya "Zima" kutazima zana ya kuingiza data. Unaweza pia kubofya zana ya kuingiza data iliyochaguliwa ili uiwashe/uizime.

Sasa umewasha zana ya kuingiza data, fungua ukurasa wa wavuti, sogeza kishale hadi kwenye kisanduku cha kuingiza, na uanze kucharaza. Isipofanya kazi, onyesha upya ukurasa wa wavuti kwa kubofya kwenye .

Makala yanayohusiana kuhusu jinsi ya kutumia zana maalum za kuingiza data: