Kuwezesha jumuiya za karibu za Zanzibar kutumia teknolojia ya Taswira ya Mtaa

Kuwezesha mchakato wa kutambulika kimataifa ni kipaumbele cha nchi yoyote ile inayotegemea utalii ili kukuza uchumi wake na Zanzibar ni mojawapo ya nchi hizo. Hivyo, lilipokuja suala la kuleta matokeo chanya ya kiuchumi katika nchi yao, Tume ya Mipango ya Zanzibar ilidhamiria kuonyesha uzuri wa visiwa vyao, na teknolojia ya Taswira ya Mtaa ilikuwepo kutoa usaidizi. Pamoja na wataalamu wa kupiga picha, Federico Debetto, Nickolay Omelchenko, na Chris du Plessis kutoka World Travel in 360 (WT360), tume ilianzisha Project Zanzibar na kuzivutia jamii za nchini ziendeleze mradi kwa kujitegemea.

Taswira ya Mtaa ya Google - Kuwezesha jamii za Zanzibar

Watch the film

Link to Youtube Video (visible only when JS is disabled)

kilomita 1700

picha zilizopigwa

elfu 980

picha zilizochapishwa

milioni 33

mara za kutazamwa

hoteli 105

zilizoorodheshwa

Kuongeza ujuzi pamoja

Kuweka maeneo yote katika ramani ni changamoto. Kwa hivyo timu ya WT360 iliungana na wanafunzi kumi na wawili wa kujitolea kutoka chuo cha State University of Zanzibar ili kusaidia kuweka eneo la kisiwa kizuri cha Unguja kwenye ramani. Wakiongozwa na utaalamu wa Federico, Nickolay na Chris, walinasa jumla ya kilomita 1,700 za video.

Utalii unachangia zaidi ya asilimia 30 ya pato letu la taifa (GDP). Hivyo, tulifanikiwa kutoa mafunzo kwa vijana wetu na wale ambao wako tayari kufanya kazi katika tasnia ya utalii. Kumekuwa na nyakati ambapo watu walichukulia utalii kuwa sekta inayohusiana na hoteli. Maana ya utalii ni pana kuliko hiyo. Una historia, una mashirika ya ndege na una upande wa masoko. Kuwa na wenyeji wengi wa Zanzibar wanaojishughulisha na sekta hii kutakuwa na manufaa makubwa kwa serikali na katika uchumi wa nchi.

-

Simai Mohammed Said, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.

Kadiri Zanzibar inavyokua, timu ya Federico huonyesha upya picha za 360 za mitaa ya Zanzibar ili kutoa usaidizi wa kuboresha miundombinu, na kuvutia watalii wengine kutembelea nchi hiyo.

Picha ya mtaa kutoka Feberico Debetto nchini Zanzibar kwenye Taswira ya Mtaa ya Google

Kutangaza biashara duniani kote kwa kutumia picha za 360

Mwanzoni mwa mwaka huu, Federico alianza kutalii kisiwa cha kaskazini cha Pemba. Ndani ya siku 6, Federico na Ibrahim Khalid, mwanafunzi wa kujitolea, walinasa zaidi ya kilomita 500 za picha na panorama 40 za angani, ambazo walizipakia kwenye Ramani za Google kwa kutumia Studio ya Taswira ya Mtaa.

Kupitia video sahihi za vivutio vya watalii, vituo vya turathi, hoteli na biashara, waliweza kuandaa National Global Tour of Zanzibar, jukwaa la picha ambalo linakua kwa kasi na linatangaza visiwa hivyo duniani kote.

Kuanzia uwekaji wa maeneo kwenye ramani hadi kutengeneza fursa za ajira

Federico alipoonana kwa mara ya kwanza na Shamymu Yassin, alikuwa mwanafunzi wa kujitolea aliyekuwa na ndoto ya kuwa mdhibiti wa ndege isiyo na rubani. Kutokana na wajibu wa kuboresha mustakabali wa Zanzibar, Shamymu aliungana na timu ya WT360 ili kujifunza kuhusu teknolojia ya Taswira ya Mtaa. Alifundishwa kuhusu kamera bora zaidi ya kutumia, jinsi ya kunasa picha na jinsi ya kuzipakia kwenye Ramani za Google. Baada ya muda mfupi, Shamymu alibobea katika ujuzi huu na akawa mtaalamu wa kupiga picha, akitalii na kuweka maeneo ya visiwa vya Zanzibar kwenye ramani ili kujipatia riziki.

Hivi sasa, Federico, Shamymu na Ibrahim wanafanya kazi ya kupakia picha mpya za angani za kisiwa cha Zanzibar, kwa kuzingatia maeneo yaliyoendelezwa hivi karibuni, biashara mpya na hoteli zilizofanyiwa ukarabati. Na kutokana na kufunguliwa kwa bustani ya burudani katika Zanzibar, dhamira yao inaendelea kukua.

Kuweka maeneo mengi ya Zanzibar kwenye ramani: uchapishaji bora na wa haraka wa data ukitumia Studio ya Taswira ya Mtaa

Ubora wa picha na kamera umeongezeka tangu mwaka 2019. Na kwa kuanzishwa kwa Studio ya Taswira ya Mtaa shughuli ya kuchapisha picha imekuwa rahisi na ya haraka. Wapigapicha wanaweza kupakia video nyingi zinazozunguka digrii 360 kwa wakati mmoja, kufuatilia hatua za maendeleo, kutafuta maudhui yaliyopakiwa kulingana na eneo au jina la faili halisi na kupanga mikusanyiko yao ya baadaye kwa kutumia maelezo wasilianifu yanayowekwa kwenye ramani.

 

Tumechapisha picha za maeneo yote ya kisiwa Pemba kwa kutumia Studio ya Taswira ya Mtaa. Maboresho makubwa ya zana ni ya kiuratibu, kama vile uwezo wa kuendeleza upakiaji uliosimamishwa au kukatizwa na kupakia video kadhaa kwa pamoja bila kuhitajika kuamka usiku ili kuweka faili mpya. Hii ilitusaidia kupata muda wa kutosha wa kulala!

-

Federico Debetto, mtaalamu wa kupiga picha

 

Kujenga fursa za siku zijazo

Mradi wa Zanzibar ulianza kwa lengo la kuwawezesha na kuwaelimisha wanafunzi wanaokaa nchini humo kuweka maeneo ya nchi yao kwenye ramani, na tangu hapo imeleta matokeo chanya zaidi duniani. Katika kipindi cha miaka mitatu, mradi huu umechochea ukuaji wa biashara za karibu na kufungua fursa za ajira kwa wafanyakazi wa kujitolea wa zamani kama Shamymu na Ibrahim.

Shiriki Picha zako mwenyewe za Taswira ya Mtaa