Programu Inayotambua Mbinu za Kuingiza Data (IME)

Programu Inayotambua Mbinu za Kuingiza Data (IME) hubadilisha micharazo ya vitufe kuwa herufi katika lugha nyingine. Tunatoa aina kadhaa za Programu Inayotambua Mbinu za Kuingiza Data (IME). Zijaribu.

Ili utumie Mbinu za kuingiza data, hatua ya kwanza ni kuwasha Zana za Kuingiza Data. Fuata maelekezo ili uwashe Zana za Kuingiza Data katika Huduma ya Tafuta na Google, Gmail, Hifadhi ya Google, Youtube, Google Tafsiri, Chrome na Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome.

Mbinu ya kuingiza data inawakilishwa na herufi kutoka lugha husika, kama vile .Kubofya ikoni ili kuwasha/kuzima Mbinu iliyopo sasa ya kuingiza data au bofya kishale kilichokaribu nayo ili uchague zana nyingine ya kuingiza data. Programu Inayotambua Mbinu za Kuingiza Data (IME) inapowashwa, kitufe hubadilika rangi na kuwa rangi ya kijivu iliyokolea.

Programu Inayotambua Mbinu za Kuingiza Data za Kilatini

Programu Zinazotambua Mbinu za Kuingiza Data (IME) za Kilatini zina lengo la kuwasaidia watu kucharaza katika lugha za hati ya Kilatini (kwa mfano, Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kireno, Kiitaliano na Kiholanzi) kwa kutumia kibodi ya Kimarekani. Vipengele ni pamoja na uwekaji wa alama maalum juu au chini ya herufi, urekebishaji wa tahajia, na kukamilika kiambishi awali.

Ili kutumia Programu Inayotambua Mbinu za Kuingiza Data (IME) za Kilatini, chapa herufi za kawaida zisizo na alama za juu, na neno sahihi na alama maalum za chini au juu ya herufi zitapendekezwa. Kwa mfano, katika Kifaransa, unapochapa 'franca', utaona pendekezo la kukamilisha kiambishi awali.

Bonyeza "TAB" ili kutumia pendekezo la "français". Kwa wakati huu, bonyeza "SPACE"/"ENTER" ili kutumia maandishi chanzo "franca".

Unapoendelea kuchapa "francais", pendekezo lililo juu, moja kwa moja, huwa pendekezo lenye alama maalum za juu au chini ya herufi. Bonyeza "SPACE"/"ENTER" ili kutumia pendekezo la "français".

Ili kuleta mapendekezo zaidi, bonyeza"BACKSPACE", na utaona mapendekezo yote.

Pendekezo la kwanza litakuwa pendekezo lenye alama maalum za juu au chini ya herufi kiotomatiki litakalofanana kwa karibu kabisa na ulichokicharaza, na litaangaziwa kiotomatiki. Pendekezo la pili ni maandishi chanzo. Mapendekezo ya tatu na ya nne ni mapendekezo ya kukamilisha kiambishi awali kiotomatiki. Mapendekezo ya 5 na 6 ni mapendekezo ya kusahihisha tahajia.

Ili kuchagua neno kutoka kwenye mapendekezo mengi, fanya lolote kati ya yafuatayo:

  • Bonyeza "SPACE"/"ENTER" ili kuchagua pendekezo lililoangaziwa,
  • Libofye,
  • Charaza nambari iliyo kando ya neno,
  • Kagua orodha ya mapendekezo katika ukurasa kwa vitufe vya "UP"/"DOWN". Pindua kurasa kwa vitufe vya "UP"/"DOWN".