Gmail

Tazama video hii ili uelewe kwa haraka jinsi ya kusanidi Zana za Kuingiza Data katika Gmail.

Ili kuwasha Zana za Kuingiza Data katika Gmail, fuata hatua hizi:

  1. Bofya ikoni ya gia iliyo sehemu ya juu kulia, kisha uchague "Mipangilio".
  2. Katika kichupo cha Jumla, chagua kisanduku kilicho kando ya "Washa zana za kuingiza data" iliyo katika sehemu ya "Lugha".
  3. Katika kidadisi kinachotokea cha mipangilio ya "Zana za Kuingiza Data", chagua zana ya kuingiza data unayoipenda kutoka sehemu ya "Zana zote za kuingiza data" na ubofye kishale cha kijivu kinachotokea katika sehemu ya "Zana za kuingiza data zilizochaguliwa".
    • Unaweza pia kubofya mara mbili zana ya kuingiza data ili uiongeze kwenye sehemu ya "Zana za kuingiza data zilizochaguliwa"
    • Unaweza kuagiza tena zana za kuingiza data zilizochaguliwa kwa kubofya zana yenyewe na kubofya kishale kinachotokea cha juu/chini
  4. Bofya Sawa katika kidadisi cha mipangilio
  5. Bofya Hifadhi Mabadiliko katika sehemu ya chini ya kichupo cha Jumla

Unapowasha Zana za Kuingiza data, utaona ikoni ya zana za kuingiza data upande wa kushoto wa ikoni ya gia, k.m..

Chapisho hili la blogu ya Gmail (lililochapishwa kote katika Blogu za Google na Biashara) linatanguliza jinsi Zana za Kuingiza Data zinavyorahisisha mawasiliano kati ya lugha mbalimbali katika Gmail.

Makala yanayohusiana kuhusu jinsi ya kutumia zana maalum za kuingiza data: